Jumatatu , 12th Dec , 2016

Msanii Mwana FA ambaye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume kwenye EATV Awards, ametoa pongezi kwa tuzo hizo, kwa kitendo cha kutoa tuzo ya heshima kwa Dj Bonny Love.

Alichopost Mwana FA

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Mwana FA amefurahia ushindi wa Dj Bonny Love huku akikumbushia historia ya maisha yake kimuziki, na kwamba bila Dj huyo asingefika hapa alipo sasa.

Pia Mwana FA amesema kufanyika kwa tuzo hizo ni mwanzo wa kuelekeo kuzuri zaidi kwenye sanaa ya Tanzania.

BJ Bonny Love akipokea tuzo ya heshima aliyokabidhiwa na Waziri Nape Nnauye

 

 

 

Tags: