Alhamisi , 15th Dec , 2016

Msanii Alikiba ametoa sababu inayomfanya akae muda mrefu bila kutoa kazi mpya, tofauti na wasanii wengi wa bongo wanavyofanya.

Alikiba (Katikati) mara baada ya kupokea tuzo

 

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio mara baada ya kunyakua tuzo tatu katika usiku wa EATV Awards, Alikiba amesema anafanya hivyo kwa ajili ya utofauti wa kazi zake na pia muziki wake una thamani kubwa sana.

“Ni kwa sababu ya utofauti tuliokuwa nao, I believe mi muziki wangu una thamani kubwa sana, kwa hiyo bidhaa yangu inapokaa muda mrefu siwezi kuleta bidhaa nyingine kwa sababu hii ya kwanza haijaisha, nataka watu wapate watosheke ili wakiridhika ndio niweze kutoa nyingine, nitapata hasara kama nitatoa bidhaa nyingine ikawa ni nzuri zaidi ya mwanzo, iliyopita ambayo haijaisha hata utamu ikaisha, nitakuwa nimejitia hasara”, alisema Alikiba.

Pia Alikiba amesema muziki kwake ni biashara na una siri kubwa, na ukifanya kwa ushindani hakutakuwa na muziki mzuri.

Tags: