Jumamosi , 9th Jan , 2016

Msanii wa muziki Kala Jeremiah, ameweka wazi kuwa muziki anaoufanya kwa sasa ndio sababu ambayo ilizima ndoto zake kubwa na kipaji cha kucheza mpira wa kikapu ambao alikuwa amedhamiria kufika nao katika ligi yake kubwa ya NBA huko Marekani.

Kala Jeremiah

Kala ameeleza kuwa, anaamini isingekuwa muziki angebakia katika upande wa mchezo huo ambao ana uhusudu mpaka sasa akiwa amebaki kama shabiki akiwa anacheza mchezo huo kwa kujifurahisha tu mtaani.

Kala ambaye kwa sasa anatamba na kazi yake mpya inayokwenda kwa jina Malkia, ameeleza pia kuwa timu ya mchezo huo ya kimataifa ambayo anaihusudu ni Los Angeles Lakers kutoka Marekani, akiwa anamuelewa sana supastaa wa kimataifa wa mchezo huo, Kobe Bryant.