Jumanne , 7th Feb , 2017

Msanii Jebby ambaye amewahi kutamba na ngoma kama 'Swahiba' akiwa ameshirikiana na mkongwe Afande Sele, amefunguka na kusema kwa sasa yupo tayari kurudi kwenye muziki baada ya muda mrefu kukaa pembeni.

Msanii Jebby akiwa kwenye studio za East Africa Radio, miaka kadhaa iliyopita.

Jebby amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EATV na kudai kuwa mpaka sasa amefikia nusu ya makubaliano pamoja na Mubenga aliyekuwa meneja wa lebo ya muziki wa bongo fleva ya Poz Kwa Poz (PKP) ambaye ameonesha nia ya kutaka kumrudisha kwenye muziki kwa sasa. 

"Nilikuwa kimya kwa muda mrefu, nimesoma vizuri game na nimefanya kazi nyingi sana ziko ndani. Saizi nikirudi narudi vizuri maana muziki umebadilika sana siku hizi video lazima ziwe kali maana zinafika mbali, hata mtu akiona huko lazima ajue kuwa kweli jamaa amebadilika siyo kama zamani. Mubenga atamrudisha Jebby kwenye muziki nimefanya makubaliano nao kwa asilimia hamsini tushakubaliana" alisema Jebby 

Aliyekuwa meneja wa label ya PKP, Mubenga.