
Willow Smith kushoto na mama yake Jada Pinkett Smith
Willow Smith amesema anampongeza mama yake kwa kuwa mkweli kuhusu suala hilo ambapo alimueleza baba yake kwamba alikuwa na mahusiano na mwanaume mwingine, na kwa upande wake anatafsiri kitendo hicho kama ni mapenzi ya kweli.
Akizungumza hilo na mama yake kwenye show yao ya Red Table Talk Willow Smith amesema "Nataka kuweka kila kitu hapa mezani, najivunia wewe kwa ulichokifanya kwa baba yangu kwa kumueleza ukweli, kwangu mimi niliona kama ni dili la ukweli na mapenzi ya kweli, nipo pamoja na wewe nitasimama na kukushika mkono kwa sababu nakupenda na wewe ni muhimu sana".
Wiki kadhaa zilizopita dunia ilfahamu kuwa msanii August Alsina alikuwa na mahusiano na mke wa Will Smith, Jada Smith ambapo watu walijaji zaidi kuhusu umri wao maana wamepishana miaka 21.