Ijumaa , 27th Nov , 2015

Msanii Peter Msechu ameeleza namna ambavyo mama wa binti yake Lauren, ni mwanamke ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika safari yake ya muziki mpaka kufika hapa alipo, akijiaminisha kuwa ataendelea kumganda na kuwa naye pamoja katika hali yoyote.

Familia ya Peter Msechu

Msechu amesema kuwa, amekutana na ubavu wake wa pili huyo mwaka 2002, na amekuwa na imani kubwa na kipaji chake tokea akiwa mwimbaji wa kanisani na hapa anaeleza namna ambavyo historia hii imeimarisha penzi alilonalo kwake.

Amariss (Mama Lauren - Lolo)