Jumatatu , 29th Sep , 2014

Wasanii wa muziki kutoka Uganda, Moze Radio na Lillian Mbabazi wameelezwa kuwa na mpango wa kufunga ndoa, baada ya ukaribu wao kuongezeka kwa kasi na familia yao kuongezeka.

wasanii wa muziki wa Uganda, Mose Radio na Lillian Mbabazi

Kwa sasa, wasanii hawa wanangojewa kutangaza tarehe rasmi ya tukio hili, ambapo Radio anakamilisha ziara yake huko Marekani wakati Lilian akimaliza ratiba zake za kimuziki huko nchini Kenya.

Wasanii hawa kwa sasa wamejaliwa kuwa na watoto wawili ambapo kwa mujibu wa chanzo cha habari, Radio anakabiliwa na msukumo mkubwa kutoka kwa familia pia, kukamilisha hatua ya kumuoa mama watoto wake huyu mara moja.