
Moustapha naye ameibuka na kusema kuwa amegombana na mpenzi wake huyo sababu ya picha aliyopiga na shabiki wake wa kike kutomfurahisha akielezea kuwa Huddah alikasirishwa sana na picha hiyo kiasi kwamba hakuwa tayari kurudisha moyo wake tena nyuma, maelezo ambayo yanapingana na ya Huddah ambaye amesema Moustapha anafahamiana naye kwa mbali na alikua akimtumia kujijengea umaarufu.
Mahusiano ya wawili hawa tangu awali yalidhihirisha kuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo havikuwa sawa sawa, ambapo wawili hawa walitangaza kuwa na ngoma waliyofanya pamoja, ngoma ambayo Huddah amesema kuwa atadai fidia endapo itaachiwa bila ridhaa yake.