Mose Iyobo alisema hayo kupitia eNewz ya EATV na kudai kuwa muziki unahitaji mtu kujipanga ili uweze kumlipa lakini siyo kukurupuka kama ambavyo Harmorapa amefanya.
"Mimi ni mtu ambaye nipo kwenye muziki muda mrefu, kila siku nyimbo mpya zinapotoka ziwe za watu maarufu hata wasio maarufu nazisikia lakini mimi sijawahi kusikia kazi yoyote ya Harmorapa, kwa hiyo sina cha kumshauri ila hiyo kazi anayofanya inahitaji mtu makini, anayeenda na wakati na siyo kukurupuka tu na kufanya ghafla sababu hiyo kazi ina pesa nyingi sana na inatia umasikini kwa haraka sana kama haufanyi vile inavyotakiwa" alisema Mose Iyobo
Hii ni mara ya pili kwa Mose, kumchana Harmorapa, mara ya kwanza, alitoa kauli ya kumfananisha harmorapa na 'nyani'