Jumatatu , 21st Oct , 2024

Rapper Moni Centrozone amefunguka kuwa kwasasa goma lake la #Pisi ndio goma kubwa Tanzania nzima kwasasa.

Pichani Ni Msanii Moni Centrozone

Mbali na hayo pia ameeleza kuwa amepitia mengi hapo kipindi cha nyuma ikiwemo kunyimwa shows pamoja na kufutiwa ngoma mtandaoni.

 

Kupitia ukurasa wake wa instagram Msanii Moni Ameandika......."Kutoka kufungiwa Akaunti (Instagram) kushushiwa ngoma mtandaoni,kunyimwa vimeo na changamoto kede kede,nilikuwa mtulivu sababu namuamini zaidi Mungu" Ameandika Moni Centrozone.

 

"Siku tano zilizopita nimetoa ngoma kubwa bongo nzima! yes ndio ngoma kubwa Tanzania, Nashukuru wasanii wenzangu pia wanajua hilo nashukuru mashabiki sana sana watoto wakike hili goma wanalala nalo wanaamka nalo."Ameandika Moni Centrozone.