Jumanne , 11th Aug , 2015

Mke wa Staa wa muziki wa Mombasa nchini Kenya Sudi Boy, Salma Lutevesi anatarajiwa kuzikwa leo kwa taratibu za kiislamu baada ya kupoteza maisha siku ya jumapili kwa maradhi ya homa ya mapafu.

Staa wa muziki wa nchini Kenya Sudi katika picha akiwa na marehemu mke wake Salma Lutevesi

Hata hivyo, mpango huo unatarajiwa kwenda taratibu na mpango wa awali kutokana na mambo ya kifamilia ambayo Sudi Mwenyewe ameahidi kuweka wazi baada ya kufikia maelewano.

Sudi Boy ambaye amesimama vizuri katika korasi ya ngoma ya Jaguar ya Barua kwa Rais, ameachiwa jukumu la malezi ya mtoto wao mmoja, na eNewz tunamtakia faraja katika kipindi hiki kigumu. Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.