Alhamisi , 14th Aug , 2014

Msanii wa muziki Bobi Wine ameendelea kukumbwa na matukio yanayohusishwa na msimamo wake kupinga ushoga, baada ya mtandao wa Youtube kuondoa video yake ya Size Yo kwa madai kuwa inachochea ugomvi.

msanii bobi Wine wa nchini Uganda

Hatua hii inakuja baada ya taarifa za awali za msanii huyu kunyimwa viza ya kuingia huko UK kufanya shughuli zake za kimuziki kutokana na msimamo wake.

Bobi Wine amesema kuwa, hatua hii haimzuii kuendelea kufanya kazi zaidi za muziki huku akiwa anaendelea kuwatayarishia kazi nzuri zaidi mashabiki wake siku hadi siku.