Ijumaa , 6th Oct , 2023

Mwanaume mmoja kutokea huko nchini Nigeria aliyefahamika kama @topic_mouth amejitokeza hadharani kwa ajili  ya kuweka jambo moja sawa, Jambo lenyewe ni kuhusiana na watu kuufananisha muonekano wake na msanii kutokea nchini humo anayefahamika kama Nairamarley.

 

Malamiko ambayo alikuwa anayatoa topic_mouth, ni kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakimshuku na marafiki zake wakimuogopa kwa kuwa muonekano wake ni kama NairaMarley, 

Hii inakuja mara baada ya sakata la kifo cha mwanamuziki ''Mohbad'' ambacho kimegubikwa na utata na moja kati ya watu wanaohisiwa kuhusika na kifo hicho ni Nairamarley. Lakini ni (mitazamo ya watu tu) hakuna uchunguzi uliyothibitisha hili.