Jumanne , 20th Aug , 2019

Miss Tanzania 2018/2019 Queen Elizabeth Makune afunguka ishu za kushirikiana na wasanii wa Bongo Movie kuzindua kampeni ya kutalii,urembo na utofauti wa maisha aliyonayo kwa sasa.

Miss Tanzania 2018/2019 Queen Elizabeth Makune

Queen Elizabeth Makune amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'Twenzetu Kutalii' ambapo amesema nia ya kampeni hiyo ni kuhamasisha watanzania wawe na utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii na risilimali zake.

"Tanzania ina vivutio vingi duniani inashika nafasi ya pili kwa ubora zaidi lakini pamoja na wingi wote huo wa vivutio na uzuri ila idadi ya watembeleaji ni wachache" amesema Queen Elizabeth.

Aidha Miss huyo amezungumzia suala la watu wengi kupenda kumtongoza ambapo amesema,

"Mimi ni mrembo na Miss Tanzania yaani nchi yote hii mimi ndio namba moja, kwa siku natongozwa mara nyingi sana na watu wa aina zote, kutongozwa ni sehemu ya mwanamke katika maisha ya kawaida na usipotongozwa itabidi ukafanyiwe maombi kanisani".

Pia ameendelea kusema yeye hana mahusiano na kigogo wowote wa serikali ila watu ndio wanasema hivyo na wala hana jibu sahihi juu ya suala hilo.