Jumamosi , 22nd Aug , 2015

Msanii wa anayetamba na wimbo Nakuwaza aliomshirikisha nguli wa muziki nchini Tanzania Bushoke, Koku Dramer amesema wasanii wengi wa mikoani licha ya kuwa na vipaji wanashindwa kufanya vizuri kutokana na soko la muziki kuegemea sana Jijini Dar.

KOKU

Koku amesema kuwa kuna wasanii wengi wanafanya vizuri mikoani lakini wanashindwa kutamba kutokana mfumo wa sasa wa media zote kubwa kuonekana ni zilizopo dar hivyo kunawafanya wengi kukosa nafasi kutokana na wingi wasanii.

Koku ambae yupo mbioni kuchai video yake hiyo na Bushoke amesema licha ya kufanya na Bushoke lakini pia ana ndoto za kufanya kazi na wasanii Engine akiwemo Barnaba au Ruby ili kuzidi kupeleka mbele muziki wake.