Jumatano , 3rd Sep , 2014

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda, amewataka wapenda burudani kujitokeza kwa wingi katika onesho la Kilimanjaro Music Tour ambalo litafanyika ndani ya manispaa yake, Leaders Club Kinondoni Jumamosi hii.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni DSM Yusuph Mwenda

Akiongea na EATV, Mstahiki Meya Mwenda amesema kuwa amependezwa na kauli mbiu ya mwaka huu ya onesho hili 'Zungusha kikwetu kwetu, ambayo inahamasisha wananchi kujivunia vya kwao.

Ameelezea kuwa tamasha hilo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuwainua wasanii wa muziki nchini kwani hii ni moja kati ya ajira kubwa ambazo wasanii wanatakiwa kutumia fursa katika kujitangaza na kujiendeleza zaidi ya hapo walipo sasa.