
Meneja Moko Biashara akiwa na msanii wake Nandy
"Ugumu ni mkubwa sana, Nandy ni mmoja wa wasanii ambao nikikupa sasa hivi labda saa 1:20 basi saa 1:29 utanirudishia utasema humuwezi, kwa sababu ni mtoto wa kike 'make up' anatumia saa mbili, kuamka lazima mpigishane kelele lakini akiamka anakuwa active"
Meneja Moko Biashara ameendelea kusema "Kitu kingine ni kwamba changamoto zake tayari nishazielewa itabidi tupambane tu, tunagombana, kuzimiana simu, wiki nzima hatusemeshani minuno tu lakini yote ni kujenga".
Aidha Moko Biashara amesema kwa sasa ana muda wa miaka mitatu tangu aanze kufanya kazi na Nandy The African Princess.