Jumanne , 16th Jun , 2015

Staa wa michano wa nchini Kenya, Mejja ameweka wazi kuwa safari yake ya muziki ambayo imemfanya kufika alipo sasa, imehamasishwa kwa kiasi kikubwa na kaka yake wa damu ambaye alikuwa akifanya muziki katika kundi lililofahamika kama Ghettoh Clan.

Mejja

Mkali huyo ameweka wazi kuwa, sehemu kubwa ya ujuzi wake ni kutoka kwa kaka yake huyo huku akiwa na mipango ya kumshawishi na kumvuta studio kufanya naye kazi pamoja kuonyesha mashabiki uwezo aliokuwa nao.

Vilevile mkali huyo wa michano ambayo kwa sehemu kubwa pia uhusisha vichekesho, amekuwa ni msingi mkubwa wa kuhamasisha wasanii chipukizi kuwa ndoto zao za kufanikiwa zinawezekana, binafsi akiwa hadithi ya kusisimua ya safari ya mafanikio ya kimuziki kutoka mwaka 2007.

Mejja akiwa na Kaka pamoja na Mama yake