Jumatatu , 27th Jul , 2015

Msanii wa miondoko ya Dancehall kutoka Jamaica, Mavado Gully hatimae sasa anatarajiwa kutua nchini Kenya kwa ajili ya kutumbuiza mashabiki waliokuwa na hamu ya kumuona star huyo mkali.

staa wa muziki wa miondoko ya dancehall nchini Jamaica Mavado Gully

Akiwa sasa katika kukamilisha makubaliano na mratibu wa tukio hilo, raia wa Kenya mwenye makazi yake huko Norway ambaye ametua Kenya kushughulikia taratibu ya kazi hiyo ameelezea kuwa mambo yote yapo sawa.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, maandalizi ya ujio wa star huyo wa kimataifa yanafanyika kwa umakini mkubwa kuhakikisha mapungufu yoyote hayatokei kama ambavyo ilikuwa kipindi cha nyuma na kufelisha ujio wake.

Show hii imekuwa na hamasa ya aina yake kwa wakazi wa Kenya, hasa baada ya ujio wa Mavado kushindikana mara mbili, mwaka 2011 na 2012 ambapo star huyo alilazimika kuomba radhi kwa mashabiki wake kutoka eneo hilo.