Ijumaa , 15th Apr , 2022

Kaka wa aliyekuwa msanii Maunda Zorro Banana Zorro amesema dada yake atazikwa siku ya Jumamosi nyumbani kwake Toangoma Kigamboni saa 10:00 jioni.

Picha ya Banana Zorro na marehemu dada yake Maunda Zorro kulia.

Banana Zorro amesema ratiba ya mazishi itaanza na misa ya kwanza nyumbani kwa baba yao Mzee Zahir Zorro Kigamboni Maweni, kisha misa ya pili itafanyika nyumbani kwa Maunda Zorro na atazikwa hapohapo nyumbani kwake.

Zaidi tazama hapa kwenye video Banana Zorro akitoa ratiba kamili ya mazishi.