Maua Sama
Maua amefunguka leo kwenye Planetbongo ya East Africa Radio, ambapo amesema anajitahidi kutosumbuliwa na presha ya Iokote kwani hata kipindi anaitoa hakujua kama itakuwa kubwa kiasi hicho.
''Unajua kuna wasanii wamepotea kwasababu ya presha za kutoa ngoma kubwa kushindanisha na iliyopita, kwangu ni tofauti sana kwasababu nimeshajiandaa kuja na muziki wangu tu kama kawaida ambao naamini utawamba mashabiki zangu'', amefunguka.
Maua ameweka wazi kuwa hakuna wimbo ulimpa presha kama Iokote kwasababu ulikuwa sio aina ya muziki wake hivyo aliamini huenda watu wakamkosoa zaidi lakini matokeo yake yalikuwa tofuati.
Ngoma hiyo ambayo ilipandishwa kwenye mtandao wa 'Youtube' Oktoba 6, 2018 tayari imeshatazamwa zaidi ya mara milioni 5 hivyo kuweka rekodi kwenye maisha yake ya muziki kwani hakuwahi kupata mapokezi makubwa ya nyimbo zake.