Jumamosi , 28th Nov , 2015

Msanii wa muziki Matonya, akiwa ndio kwanza ameachia rekodi yake mpya ya malavidavi inayokwenda kwa jina Jela, amezizima hisia kuwa rekodi hiyo inabeba kisa cha kweli kuhusiana na mahusiano yake.

Matonya

Matonya katika mahojiano exclusive ya kutambulisha mkwaju huo rasmi kutoka shoo ya Planet Bongo East Africa Radio , ameeleza kuwa, ameamua kuzungumzia mapenzi bora katika picha kubwa ya Jela ya mapenzi, ambapo wapendanao wote wanaweza kujifungia na kuimarisha mapenzi yao.

Staa huyo amewataka mashabiki wake kuelewa kuwa, rekodi hiyo ambayo imefanywa na Sheddy Clever, Burn Records ni kazi ambayo anaitazama kama shilingi ya Nyerere, akitaka sapoti kwa mashabiki ili kufikisha kazi hiyo mbali.