Ijumaa , 18th Dec , 2015

Msanii Izzo Buzness ambaye ameachia video ya wimbo wa shem lake, anakabiliwa na wakati mgumu baada ya mashabiki wengi kuonyesha kutofurahishwa na video hiyo, wakimtuhumu kuwa director hajaitendea haki.

Mashabiki hao wametoa maoni yao kwenye mtandao wa Youtube baada ya kuangalia video hiyo, na kusema kuwa imekuwa tofauti na walivyotarajia, kutokana na wimbo wake kuwa mzuri.

“Daah sasa ndio manaake nini Emmanuel a.k.a Izzo?..wewe ndio umeandika hii script ya video au huyo Khalfani? yaani director umefanya kutuonesha big boots na maghorofa na swimming pool sasa kama mlikuwa mnataka kutuonyesha hayo kwanini msingefanya ngoma ya ku_bang mtuonyeshe hayo yote?????????? ngoma kali ila haifanani na script hiyo mliotumia kufanya video kiukweli yaani concept ya huyo shemeji uliemtaja haipo kabisa apo mmetujaza”, alisema Kasaloo Junior kwenye maoni yake.

“Katika video zako zote izzo businesses kiukwel hii umechemsha kila kitu...sijaifurahia hata kidogo... But location rangi ya video nzuri but editing mbovu....the way camera kama inacheza haijatulia..... but big up nakuaminia bro... audio ipo gud bt video umechemsha i dea yake sjaipenda kabisa”, alisema shabiki mwingine alitambulika kwa jina la Kelly Shio.

“Video nzuri, location nzuri, rangi nzuri lakini vitu 2 dir kachemka. 1- G Nako ameiga style ya kuvaa kama Wiz Khalifa, 2- hakuna concept ya ushemeji katika hii video", aliandika Mshanga F.

“Umefeli tena Izzo b”, alisema Juma Ramadhani.

Tukumbuke hivi karibuni kulikuwa na malalamiko toka kwa baadhi ya Directors wa hapa nyumbani kuwalalamikia wasanii kwenda kufanya kazi na Director wa nje, wakati hapa nyumbani kuna watu wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa kiwango sawa na wa nje.

Video hiyo imeachiwa rasmi jana na imetengenezwa na Director Khalfani, hivyo timu ya East Africa Radio itawatafuta wahusika kujibu tuhuma hizo, na sikiliza Planet Bongo ya leo ya East Africa Radio kusikia walichojibu.