Jumamosi , 14th Apr , 2018

Mara nyingi kumekuwepo na mijadala mbalimbali juu ya aina ya vazi gani linafaa kuvaliwa na jinsi ya kike au ya kiume kwa mujibu wa maadaili, lakini kwa mwimbaji wa Injili nchini Martha Maipaja yeye hana tatizo na hilo.

Akiongea kwenye kipindi cha Kikaangoni mwimbaji huyo amesema kila mtu avae kutokana na malezi aliyolelewa nayo, kama ni binti ameelekezwa kuvaa suruali sio dhambi na avae na kwa yule aliyeelekezwa kuvaa suruali ni dhambi na asivae.

''Mengine ni maisha tu ambayo hayana kifungo kwa mtu lakini unavaa kutokana na uonavyo wewe kwa mfano mimi sivai nguo ndefu sana lakini haimanishi hazina maadili kwahiyo ni wewe mwenyewe tu unaamuaje'', amesema.

Aidha Martha ameongeza kuwa hana jibu sahihi sana ila tu anachojua ni kitabu kitakatifu yaani Biblia kimeandika mwanamke asivae vazi limpasalo mwanamume hivyo kwa watalaam wa maandiko wanaweza kufafanua mavazi hayo ni yapi.