Jumatatu , 1st Aug , 2022

Msanii Afande Sele amemzungumzia bondia anayetrend kwa sasa nchini Karim Mandonga kwa kusema anapenda sana kula chips na kufanya mazoezi.

Kushoto ni bondia Karim Mandonga, kulia ni msanii Afande Sele

Kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio Afande Sele amesema 

"Mandonga alikuwa Watu Pori, nilikuaga nasafiri naye kwenye show tukifika hotelini anajifungia chumbani anafanya mazoezi, siyo mtu wa mitungi nyie mkiagiza bia moja yeye anaagiza chipsi mayai, kwa hiyo ukinywa bia 10 na yeye anakula chipsi sahani 10'' - Afande Sele