Alhamisi , 21st Jan , 2016

Kiongozi wa kundi maarufu la muziki nchini la Survival Sisters linalowakilishwa na wanadada watatu ambao ni walemavu wa viungo Bi. Irene Malekela, ameelezea ukimya wa kundi hilo umesababishwa na malezi ya mwanaye huku akiweka kando muziki.

Kiongozi wa kundi maarufu la muziki nchini la Survival Sisters, Irene Malekela

Irene ambaye anaungana na wasanii wenzake wa kundi hilo wakiwemo Lucy Samson na Latifha Abdallah, ameongea na eNewz kuwa licha ya ukimya huo, hivi sasa wanafanya juu chini kuweza kupata wadhamini kwa ajili ya kutengeneza video ya wimbo wao mpya uliobatizwa jina 'Kitchen Party'.