Jumanne , 5th Mei , 2015

Staa wa muziki Makamua, ametangaza ujio wake mpya kwa upande wa uigizaji akiwa moja ya washiriki katika projekti kubwa ya filamu unavyokwenda kwa jina Bongo na Fleva.

msanii wa bongofleva nchini ambaye sasa ni muigizaji filamu Makamua

Makamua amesema kuwa ndani yake inahusisha pia mastaa wengi na wakubwa kabisa kutoka tasnia ya muziki wa Bongo Flava, ambapo mpaka sasa projekti hiyo imekwisha kamilika.

Ameongezea kuwa hatua ya kuifikisha kwa wananchi ipo katika mipango ambayo inachukua muda kidogo kutokana na ukubwa wake, na kuhusu hili, staa huyo anaeleza zaidi hapa.