Jumatatu , 31st Aug , 2015

Majaji wa Dance 100% Queen Darleen, Shetta na Super Nyamwela kwa nyakati tofauti wamelitaja kundi la Majokery kama moja ya makundi ambayo onyesho lao lilikuwa ni la kusisimua.

majaji wa mashindano ya Dance 100% 2015 Super Nyamwela, Shetta na Queen Darleen

Hii inakuwa kama sehemu ya kipimo cha kiwango cha maonesho ambayo madansa wanayafanya katika kujitafutia alama kuelekea fainali ya Dance 100% 2015 kwa mwaka huu.

Mara tu baada ya kushuka katika jukwaa lao la kufanyia maamuzi, majaji wakakutana na eNewz na katika kujibu kile kilichowakonga nyoyo zao, show hiyo ya vijana wa Majokery ambayo unaitazama hapa pia kwa kifupi, ikiwa ikiwa na burudani iliyowafurahisha zaidi. MAJAJI DANCE100% WAVUTIWA NA MAJOKERY.