Jumatatu , 13th Nov , 2023

Rapa na Muimbaji wa Kenya Sylvia Ssaru amezua gumzo mitandaoni baada ya kuweka wazi thamani ya mahari yake akitaka kuolewa ambayo ni Ksh Bilioni 1 na kuendelea sawa na Tsh Bilioni 16 na ushee.

Picha ya Ssaru

Ssaru amefunguka hilo mbele ya waandishi wa habari wakati anafanyiwa Interview akisema

"Sitaolewa saa hii nipeni muda wa miaka kadhaa lakini kila mwaka bei inapanda ni kama Bilioni hivi. Kwani kulipia Bilioni mtu kama mimi ni tatizo".

Msanii huyo ameshakuja Tanzania kufanya Media Tour mwaka huu na amemtaja Darassa na Young Lunya kama rapa ambao anatamani kufanya nao kazi.