
Baadhi ya wasanii kutoka Tip Top Connections, kutoka kushoto ni Madee, Dogo Janja na Tuma Man
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo Madee anasema sababu kubwa kutotoa kazi kama kundi ni kutokana na biashara kwani saizi kila msanii anaangalia zaidi maslahi yake kuliko kundi na inakuwa inalipa zaidi kufanya kazi kama 'Solo Artist' kuliko kufanya kazi kama kundi.
"Tunaona hata mbele makundi kibao yanasambaratika watu wanafanya kazi kivyao vyao, saizi unakuta naweza kuitwa kwenye show pekee yangu nikalipwa milioni tano na mtu akihitaji kundi zima anaweza kutoa pesa hiyo hiyo so kibiashara inakuwa inalipa zaidi msanii kusimama kivyako. Kwa hiyo Tip Top Connection saizi tumebaki kama familia ila si biashara, tutatoa kazi ya Tip Top Connection sababu tu watu wame'miss' kusikia kazi ya kundi ila si kwa ajili ya biashara" alisema Madee.
Mbali na hilo Madee ameweka wazi kuwa tayari kuna kazi wamefanya kama kundi wamemshirikisha Diamond Platnumz na kusema kuwa siku yoyote ile wanaweza kuiachia kwa ajili ya mashabiki zao.