
Jaji wa Dance100 Khalila akiwa anaonyesha alama kwa kundi lililoshiriki shindano.
Katika makundi yote yaliyoshiriki siku ya kwanza kulikuwa na binti mmoja tu kutoka kundi la D.D.I jambo ambalo lilionyesha wazi kwamba mwitikio kwa upande wa wasichana bado ni mdogo ukilinganisha na wanaume hivyo mabinti wameaswa kujitokeza kwa wingi
Akizungumza na EATV kuhusu jambo hilo mmoja wa majaji wa kike Khalila amesema wazazi wanatakiwa kutambua kwamba sanaa inalipa na hivyo wawaruhusu watoto wao kushiriki katika shindano hilo
‘’Wazazi wanatakiwa kuwapa nafasi vijana wao kwani ukiachilia mbali zawadi ambazo zitatolewa pia shindano hili hutizamwa na watu wengi hivyo inawapa nafasi ya kutambulika na wasanii na bendi mbalimbali ambapo huwafuata na kufanya nao kazi’’. Amesema Jaji Khalila