Jumanne , 15th Sep , 2015

Rapa Mabeste anayejipanga kwa ujio wa kazi kubwa wiki ijayo, baada ya ushiriki wake katika filamu kubwa ya Wake Up, ameeleza kuwa kwa upande wake fani hiyo ni kitu ambacho amekifanya kutoa sapoti tu akiwa bado hajajikita sana katika fani hiyo.

Mabeste amesema kuwa kazi hiyo imeshirikisha mastaa wengi kutoka sanaa ya filamu na muziki, pembeni ya hilo binafsi akiwa anajipanga kutoka na projekti ya video za rekodi zake ambazo aliziachia kipindi cha nyuma bila video.