Ijumaa , 18th Sep , 2015

Wakati asilimia kubwa ya wasanii wa muziki na filamu hapa Tanzania wakiendelea kujikita katika shughuli za kampeni, nyota wa muziki M2THEP, ameweka wazi kuwa kwa upande wake anasimamia kutaka mabadiliko, bila kusimama upande wowote ule.

msanii wa bongofleva M2TheP

M2THEP amesema kuwa, akiwa katika nafasi ya watanzania walio wengi mitaani, wanasiasa wanatakiwa kufahamu kuwa mabadiliko ndio kitu cha muhimu kinachohitajika baada ya kuchoshwa na hali ngumu ya maisha, itikadi ya vyama ikiwa si kitu muhimu kwake kwa sasa, akiwataka vijana kwenda sawa na mchakato na kisha kupiga kura.