Alhamisi , 26th Nov , 2015

Rapa mkongwe katika game ya Bongo Flava, Luteni Kalama aliyejijengea jina kubwa kutoka kundi la Gangwe Mobb, ameweka wazi hatua kubwa aliyopiga kimuziki baada ya kupata lebo kutoka nchini Ufaransa, 20K Records ambayo itakuwa ikiendesha kazi zake.

Rapa mkongwe katika game ya Bongo Flava, Luteni Kalama

Akiwa chini la lebo hiyo tayari Luteni Kalama amekwishaanza kutikisa chati na kazi ya kwanza ambayo inakwenda kwa jina The Way I Feel akishirikiana na msanii Jerry Juliani anayefanya kazi zake huko Ufaransa, kazi yake ya kwanza yenye kiwango cha kimataifa.

Kuhusiana na hatua hiyo kubwa katika muziki wake Luteni kupitia mahojiano na eNewz anaeleza hapa.