Jumanne , 21st Oct , 2014

Kamati ya Miss Tanzania imesema kuwa haiwezi kumvua taji Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu kwa kuwa ni mrembo halali na mwenye vigezo vyote vilivyotakiwa, na amewataka watu kutoropoka kwa kuwa hawajui vigezo vinavyotakiwa.

mratibu wa shindano la Miss Tanzania Hashim Lundenga

Akifafanua kuhusu suala la umri, mratibu wa mashindano hayo Hashim Lundenga amesema kuwa cheti halali walichonacho wao ni kile kinachoonesha Sitti Mtemvu kazaliwa 24 Mei 1991 na si vinginevyo.

Kuhusu suala la passport na leseni zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha amezaliwa mwaka 1989, Lundenga amesema wao huwa hawangalii vitu hivyo wanachojali ni cheti cha kuzaliwa.

Lundenga pia amezungumzia tuhuma mwili wa unene wa Sitti ambapo amesema wao huwa hawaangalii wembamba wala ufupi, muhimu ni awe na vigezo vinavyotakiwa.