Alhamisi , 9th Oct , 2014

Kutokana na tatizo endelevu la mashindano mengi ya kutafuta vipaji vya kuimba kushindwa kuendeleza wasanii wanaowaibua katika sanaa hiyo, msanii Linex Sunday amesema kuwa tatizo hilo linachangiwa na wasanii hawa kukosa muongozo na uelewa wa soko.

msanii wa muziki wa bongofleva nchini Linex

Linex ambaye anajipanga na ujio mwingine mkubwa kabisa hivi karibuni, ameshauri kuwa kuna umuhimu mkubwa wa waandaaji wa matukio haya kuwekeza muda pia wa kulea vipaji hivi kabla ya kuwaacha wajiendeleze wenyewe.