Alhamisi , 30th Jul , 2015

Staa wa muziki Linah ambaye anajiandaa kumaliza wiki na mkono mpya unaokwenda kwa jina 'No Stress', amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, hii ni kazi ambayo ndani yake ameamua kuanika hisia zake zote katika mahusiano yake ya kimapenzi.

staa wa muziki wa bongofleva nchini Linah Sanga

Linah ambaye kwa sasa anaonekana kujiachia na kuwa katika furaha ya penzi na Williams Bugeme, mwanamitindo, mwigizaji na mjasiriamali ambaye amefanikiwa kuutuliza moyo wa staa huyo, anakuwa ndio mchango mkubwa kwa Linah kuwa huru sasa kutoka na rekodi inayokwenda kwa jina 'No Stress'.

Video ya kazi hii imetayarishwa huko Afrika Kusini na Director Godfather, na tayari msanii huyo amekwishakanusha uvumi kuwa Baby wake, Boss Mutoto Clemence atatokea ndani ya video yenyewe.