Jumamosi , 2nd Oct , 2021

Ndege mnana, Linah ameendelea kuonyesha ufundi wa hali ya juu kwenye muziki wa Bongo Fleva na kwenye wimbo wake mpya “Kama Yeye” anaelezea namna anavyokoshwa na mwanaume wake ambaye amefanikiwa kutibu majeraha ya mahusiano yaliyopita.

Picha ya Msanii Linah

Linah anasema “hajaona kama yeye, walipochana ameshona, hamgombezi ila ana mnong’oneza” hali ambayo marafiki zake wanahisi amemroga mpenzi wake huyo.