Jumatatu , 10th Mar , 2014

Msanii Lilian Mbabazi baada ya stori za yeye kuwa na ujauzito wa pili kuanza kusambaa kwa kasi hivi karibuni, hatimaye amejitokeza mwenyewe hadharani na kuonekana dhahiri kuwa ni kweli ana ujauzito na anatarajia kujifungua hivi karibuni.

Msanii huyu akiwa na gauni refu jeusi lililoonyesha dhahiri ujauzito wake, mwishoni mwa wiki pia aliwapatia mashabiki wake ladha kwa kufanya onyesho katika maalum kwa ajili ya kuhamasisha Wanawake katika mwezi huu ambapo wameadhimisha siku yao rasmi duniani.

Ujauzito huu wa Lilian kwa asilimia nyingi unatajwa kuwa ni kutoka kwa msanii Moze Radio ambaye ni baba wa mtoto wake wa kwanza, japo bado msanii huyu hajathibitisha rasmi swala hili.