Picha ya Lil Wayne
Kwa mujibu wa TMZ Carlos Christian aliwaambia polisi kuwa Lil Wayne alifanya tukio hilo hilo Disemba 2021 nyumbani kwake Hidden Hills, California wakati wakiwa kwenye mzozo.
Nyaraka za mahakama zinadai Carlos aliingia gharama za matibabu, alipoteza mshahara na alipatwa na mfadhaiko wa kihisia kutokana na tukio hilo pia amemshtaki Lil Wayne kwa kudai fidia na adhabu.
Kwa upande wa vyanzo vya Lil Wayne vimekanusha mashtaka hayo kwa kusema rapa huyo hakuwa na silaha na tukio hilo halijawahi kutokea.