Ijumaa , 10th Mar , 2017

'Produce'r Lamar kutoka ‘Fishcrab Record Label’ amewachana ma'producer' wa sasa kwamba wana majivuno kiasi cha kushindwa kushirikiana, jambo ambalo limesababisha nyimbo zao zote kufanana tofauti na ilivyokuwa kwa upande wao miaka iliyopita.

Producer

Akizungumza leo kwenye heshima ya bongo fleva katika kipindi cha Planet Bongo East Africa Radio, Lamar amesema muziki wa sasa hauna ladha ya tofauti kwani waandaji wamekosa ubunifu na chanzo cha yote ni wao kwa wao kutopendana na kushindwa  kubadilishana mawazo.

"Producers wa sasa wana kitu wenyewe wanakiita 'ego' kiasi kwamba wanashindwa hata kupatiana ushirikiano  ndiyo maana ukisikiliza wimbo huu unafanana na ule, hata ule mzuka ambao zamani ukisikiliza nyimbo unapata hakuna, lakini zamani ukisikia wimbo alofanya Majani, Dunga au Master Jay lazima kuna kitu cha tofauti utakipata". Alisema Lamar

Aidha Lamar ameongeza kuwa zamani waandaji wa muziki wengi walikuwa na upendo na walikuwa na uwezo mkubwa ndiyo maana hata yeye aliweza kufanya kazi na P-Funk Majani ambaye watu wengi wanamuheshimu kutokana na uwezo wake mkubwa.

"Zamani Majani mpaka akukubali ufanye naye kazi inabidi uwe na adabu lakini pia uwe na kitu cha pekee cha kumshawishi ndiyo maana hata nilivyoondoka kwake niliweza kufanya kazi na Dunga na waandaji wengine wanne tofauti kitu ambacho kilinipa ujuzi mkubwa kabla ya kuanzisha lebo yangu mwenyewe". Lamar