
Haya yamebainishwa wazi na mwimbaji wa muziki wa dance na taarabu nchini Bwana Niyonzima Omary a.k.a Papaa Fololo ambapo amebainisha wazi jinsi ambavyo ameanza harakati za kusaka maisha kuanzia miaka ya 1980 hadi hapa alipo hivi sasa.
“Nimepitia bendi nyingi sana kama vile super star, Ukonga bendi ,Five Star, japo mambo hayakwenda vizuri bendi zikawa zinasambaratika kutokana na masilahi kutokuwa vizuri na wanamuziki kukimbilia bendi nyingine”
Mwaka 1990 hadi 1994 Niyonzima alijiunga na kituo cha utangazaji huko Burundi na kufanya kazi kwa miaka minne baada ya hapo ikatokea suala la kutokuwepo na maelewano ikambidi kuja Tanzania na kuingia katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu huko Kigoma na kuendelea na kipaji chake cha uimbaji wa dance pamoja na taarabu.
"Mwaka 2014 nilifanikiwa kwenda Canada kuonyesha vipaji vyangu na kujifunza zaidi muziki wa dance na taarabu ambapo sasa hivi nina bendi mpya ijulikanayo kama Fololo ambapo nina albam yenye nyimbo kama Mama nihurumie, Kila mtu na wake, Naumia moyoni na Chuki ya nini. Alisema Niyonzima
Ujumbe ambao ninautoa kwa mashabiki zangu ni kwamba malengo yanaweza kutimia kutokana na kujituma na kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa kirahisi na kwa kufanya hivyo matokeo chanya huweza kupatikana kiurahisi.
