Ijumaa , 18th Jul , 2014

Mwanamuziki nguli wa miondoko ya taarab nchini Khadija Khopa almaarufu kama Malkia wa mipasho amejiandaa kufanya kazi na wasanii wa miondoko ya bonofleva huku akiweka wazi nia yake ya kufanya kazi na msanii Diamond Platinmuz.

Mwimbaji wa taarab nchini Khadija Kopa

Khandija Kopa ameongea na enewz kuwa anatarajia kushirikiana na wasanii mbalimbali wa miondoko hiyo wakiwemo Ommy Dimpoz, Ali Kiba, Cassim Mganga, Chidi Benz na wengieno wengi baada ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kuisha.

Khadija pia anatarajia kuzizindua albamu zake mpya mbili zikiwemo 'Lady with Confidence' pamoja na 'Kantangaze akutangaze nani wakati hata mtaa wa pili hujulikani' na pia anajiandaa kuizindua bendi yake maalum kwa ajili ya watoto wake ambao nao watakuwa wakiimbia bendi hiyo.