Jumamosi , 16th Aug , 2014

Kilimanjaro Music Tour 2014, leo hii inatarajiwa kuwasha moto wa burudani jijini Dodoma, ndani ya Uwanja vya Jamhuri kupitia show kali ambayo milango yake inafunguliwa mida hii.

Weusi ndani ya Dom taayri kukinukisha leo

Jukwaa litatikiswa na mastaa wanaotikisa gemu ya muziki Bongo akiwepo mwanamuziki Christian Bella, Rich Mavoko, Madee, Malkia wa mipasho Khadija Kopa, Mwana Fa, Mwasiti, Shilole, Weusi, Izzo Bizness na Ben Pol.

Kama kawaida, milango itafunguliwa saa 10 jioni, na kiingilio katika show hii kali ni shilingi 3,000 tu, ambapo mlangoni unazawadiwa kinywaji kimoja buree.

Dodoma mpo tayari maana hii si ya kukosa kabisa, na sasa ndio mida y kusogea pale Jamhuri. Kili Music Tour 2014, Zungusha Kikwetukwetu.