Ijumaa , 3rd Jul , 2015

Baada ya kauli ya staa wa Uganda Bebe Cool kuwa msanii mwenzake kutoka nchi hiyo, Eddy Kenzo ni msanii anayechipukia, Kenzo ameonyesha weupe wa roho yake kwa kumuombea Bebe Cool kura kwa mashabiki katika tuzo za kimataifa anazowania.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Eddy Kenzo

Kenzo ambaye ni mpikaji wa ngoma ya Sitya Loss kati ya nyingine kali anatarajia kurejea Uganda akitokea Marekani Julai 8, amewashukuru mashabiki kwa kumuwezesha kushinda tuzo kutoka BET, akitaka waonyeshe sapoti hiyo hiyo kwa Bebe Cool pamoja na Chameleone ambao wapo katika kinyanganyiro cha tuzo kubwa kabisa Afrika.

Kufuatia wengi pia kumtafsiri Bebe Cool tofauti kwa kumuita Eddy Kenzo msanii anayechipukia, staa huyo amejaribu kutoa ufafanuzi kuwa, alichokimaanisha kwa maneno hayo sio dharau bali ni kipengele tu ambacho amemuweka.