Jumatatu , 29th Dec , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda Kenzo ameonesha furaha yake kubwa baada ya mpenzi wake ambaye pia ni msanii, Rema kujifungua mtoto wa kike aliyepewa jina la Aamaal.

wasanii wa Uganda Eddy Kenzo na mpenzi wake Rema

Kenzo atakuwa amejaaliwa kupata mtoto wa pili baada ya awali kuzaa na mpenzi wake wa zamani kabla ya kuanza mahusiano mapya na Rema.

Kenzo amemshukuru Mungu na hivi sasa anakuwa ni mzazi wa watoto wawili wa kike ambao ni Maya na Aamaal.