Ijumaa , 14th Mar , 2014

Msanii wa miondoko ya Dancehall wa nchini Jamaica, Vybz Kartel ambaye amekuwa kizuizini kwa muda sasa kwa mashtaka ya mauaji ya Clive Williams 'Lizard' mwaka 2011, amepatikana na hatia katika kosa hilo baada ya siku 65 za kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Kartel amethibitika kuhusika na tukio la kuua kwa kumshambulia na kumpiga Marehemu Lizard akishirikiana na wenzake watano, ambao wote kwa pamoja watafika mahakamani tarehe 27 mwezi huu kwa ajili ya kusomewa hukumu yao.

Tukio hili limetokea kugusa watu wengi katika ngazi ya kimataifa, wakiwepo mastaa wakubwa hasa kutokana na umahiri wa Vybz Kartel katika jukwaa la muziki wa kimataifa, ambapo amekwishafanya kazi na mastaa kama vile Pitbull, Missy Elliott, Rihanna kati ya wengineo.