Jumanne , 8th Apr , 2014

Mama wa aliyekuwa msanii mahiri wa filamu Tanzania, Marehemu Steven Kanumba ameadhimisha siku ya Kanumba Day kwa kutoa msaada katika kituo cha CHAKUWAMA Jijini Dar es Salaam, kituo ambacho Marehemu Kanumba alikuwa na utaratibu kusaidia mara kwa mara.

Mama Kanumba

Katika zoezi hili, mama wa msanii huyu akiwa ameambatana na baadhi ya wasanii wa filamu hapa Tanzania, akapata nafasi ya kusikia shairi ambalo watoto hawa walimuandalia, shairi ambalo liliweza kugusa hisia zake kiundani.

Katika mahojiano ambayo eNewz tumefanya na Mama huyu, akafafanua juu ya zoezi hili la kumuenzi Kanumba kwa matendo na kusema kuwa kuendeleza kila mwanae alichokuwa anakifanya kinamsogeza karibu naye zaidi.

Katika msafara huo, Mzee Chilo alikuwemo ambapo kwa niaba ya wasanii wengine wa filamu Tanzania, akazungumzia pia kidogo juu ya umuhimu ya kutoa misaada kwa watu wanaohitaji na kusema kuwa watu wote wenye uwezi hususan wasanii wanatakiwa kukumbuka wale wanaoishi katika mazingira magumu.