
Miss Tanzania 2013-2014 Happyness Watimanywa
Gharama hizo kubwa ambazo mama Amina alizoweka wazi ni zile za kumwandaa mrembo huyo kuelekea mashindano ya Miss World mwishoni mwa mwaka huu.
Mama wa Mrembo huyu amesema kuwa, yeye binafsi amekwishagharamia mambo kadhaa katika kuhakikisha kuwa mrembo huyu anakwenda vizuri katika mashindano hayo kwa ahadi ya kurudishiwa gharama hizo kutoka kwa kamati, na mpaka sasa amekuwa akizungushwa wakati muda wa mrembo huyu kwenda katika mashindano haya umekwishafika.
