
Msanii wa Bongo fleva Quick Racka na Star wa Bongo muvi Kajala Masanja
Akizungumza na Enewz Quick Racka alisema kuwa yeye na bongo muvi star huyo ni washikaji wa karibu sana na urafiki wao una miaka miwili sasa, huku kila mtu akiwa na kazi zake.
“Tunashauriana yaani kama washikaji na nampenda kama mshikaji wangu kama hamuelewi hata picha hamuoni”,alisema Quick Racka huku akiongezea kuwa kwasasa studio yao ya switch inafanya kazi ya kumsimamisha producer wao Rufe ajulikane ndipo watakaporudi kujihusisha na msanii mmoja mmoja", alisema Quick Rocka.
Rapper Quick Rocka ambaye kwa sasa anafanya kazi na Switch Records, pia ameelezea mipango yake ya kufanya muziki wa aina tofauti tofuti, huku tetesi zikisema sasa anataka kufanya muziki wa bolingo.